Jumanne, 26 Januari 2016

Yusuph Manji Amuita Mezani Tajiri Wa Simba

INGAWA uongozi wa Simba umejibu na kufafanua kwa hoja juu ya kupinga uwekezaji wa bilionea,

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji.

ADVERTISEMENT

INGAWA uongozi wa Simba umejibu na kufafanua kwa hoja juu ya kupinga uwekezaji wa bilionea, Mohammed Dewji ‘Mo’, baadhi ya mashabiki wanaonekana kutofurahia hali hiyo huku Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, akiwasihi wakae naye (MO) mezani na kama kuna uwezekano wampe timu akumbane na mziki wake.

Manji anaamini kwamba MO akipewa Simba ushindani utaongezekana na uwekezaji utakuwa mkubwa ingawa atakumbana na changamoto nyingi kuliko anavyodhania ni rahisi akiwa nje ya Simba.

Bosi huyo wa Yanga, ametamka kwamba ujio wa Dewji Simba ungeleta changamoto kubwa ya kimaendeleo kwenye maendeleo ya soka haswa kwa watani wa jadi, lakini hamaanishi kwamba anamhofia.

“Napenda changamoto nimesikia hizo taarifa za ujio wa MO sijajua zimefikia wapi kuna wakati nilisikia ameamua kuachana na huo mpango, mimi namkaribisha wala siwezi kuhofia kwa lolote, napenda changamoto,” alisema Manji ambaye amethibitisha kugombea uenyekiti wa Yanga kwa mara nyingine kwenye uchaguzi ujao.

“Kuna changamoto kubwa katika kufanya mambo ambayo anayataka kwenye Simba, si jambo rahisi lakini naamini hata akipewa Simba bado hawezi kutupa athari zozote sisi kama Yanga,”alisisitiza  Manji na kusema ni jambo zuri kama Simba wakikaa mezani na Dewji na kumpa nafasi akumbane na changamoto za uendeshaji.

AMTAJA HANSPOPE

Manji amedai kushangazwa na hatua ya Simba mpaka sasa kuendelea na Kamati ya Usajili na viongozi wao kuwa na majukumu wakati kazi yao imeshapita. Alisema majukumu ya kamati ya usajili yanafikia tamati ligi inapoanza ambapo kamati hiyo na viongozi wake hawakutakiwa kutumia cheo hicho kwa sasa wakati majukumu yao ya kusajili yalishamalizika.

“Nasikia kuna kamati ya usajili Simba inafanya nini mpaka sasa? Sidhani kama hiyo ni sahihi majukumu yao yalishamalizika. Huoni hapa Yanga mtu anayehusika na usajili anaongea wakati huu,” alisema Manji ambaye maneno yake yameonekana kumlenga Zacharia Hanspope aliye Mwenyekiti wa Kamati ya usajili Simba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni