Jumapili, 31 Januari 2016

Navy Kenzo Waachia Video yao Mpya

Video mpya kutoka kwa kundi la navy kenzo

Noma sana:Messi Kuanza kupokea bilioni 1.7 kwa wiki

KUFURU: Messi kuanza kupokea Sh 1.7 bilioni kwa wiki

SOKA linaelekea wapi? Hakuna anayejua. Lakini sasa imefika mahala ambapo mchezaji mmoja

ADVERTISEMENT

SOKA linaelekea wapi? Hakuna anayejua. Lakini sasa imefika mahala ambapo mchezaji mmoja anakaribia kulipwa dau la Sh1.7 bilioni kwa wiki kwa mujibu wa mshahara wake.

Staa wa Barcelona, Lionel Messi ambaye ni mmoja kati ya wachezaji wa kihistoria duniani anakaribia kulipwa dau la Pauni 583,000 kwa wiki ambazo ni sawa na Shilingi za Tanzania 1,778,120,000 kwa wiki na hivyo kuweka rekodi ya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani.

Dili hilo litamfanya Messi alipwe dau la Pauni 30 milioni kwa mwaka na hivyo kumfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi kwa sasa wakati huu akiwa ameweka rekodi ya kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia mara nyingi zaidi. Mara tano.

Hilo litafanyika mwishoni mwa msimu katika kipindi cha majira ya joto wakati mkataba wa mchezaji huyo utakapoongezewa vipengele upya baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili ya nyongeza mwaka 2013 na mkataba huo unakoma mwaka 2018. Kwa mujibu wa kipengele kimoja cha nyaraka za mkataba wa Messi, imeandikwa kuwa mshahara wake utapandishwa mara mbili kuanzia mwanzoni mwa msimu 2016 bila ya kusaini mkataba mpya kutoka kwa huu wa sasa unaoisha 2018.

Kwa sasa Messi anaingiza dau la Pauni 17 milioni kwa mwaka lakini kwa mujibu wa mkataba huo, dau hilo linapaswa kwenda mpaka Pauni 29.8 milioni na hivyo kuzikata maini klabu mbili tajiri za Manchester City na PSG ambazo zinadaiwa kuwa katika nafasi ya kumtwaa Messi.

Dau la mshahara ambalo Manchester City walikuwa wamepanga kulitoa kwa Messi kwa sasa litakuwa pungufu kwa mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki lakini matumaini ya kumnasa Messi yanazidi kukatika zaidi baada ya kugundulika kuwa kama Barcelona ikiamua kumuuza staa huyo, basi suala hilo litakuja akiwa katika mshahara mpya.

ADVERTISEMENT

Kwa mujibu wa mkataba huo, Barcelona italazimika kulipa dau la Pauni 15 milioni kama fidia kwa Messi kama ikiamua kumuuza kabla ya nyongeza hiyo ya mshahara haijaanza kufanya kazi.

Licha ya dau hilo la mshahara, kwa mujibu wa Jarida la France Football la Mei 2015, Messi mwenye umri wa miaka 28 anadaiwa kukusanya kiasi cha Pauni 48 milioni kwa mwaka 2014 ukijumlisha na bonasi zake mbalimbali, mshahara na mikataba ya kibiashara.

Mauzo ya sura yake katika mikataba yake ya kibiashara kama Turkish Airlines, Fifa video Games na mingineyo yamemwongezea dau la Pauni 1.8 milioni kwa mwaka na hivyo kufikia idadi ya Pauni 21 milioni kwa mwaka.

Messi ambaye anakaribia kufikia rekodi ya staa wa zamani wa England, David Beckham ya kumaliza nafasi hiyo ya juu kwa utajiri kwa mwaka wa sita mfululizo, bado amemwacha mbali mpinzani wake wa karibu wa uwanjani, Cristano Ronaldo wa Real Madrid licha ya Ronaldo kuongeza mapato yake kwa wingi katika kipindi cha miezi 12 iliyopita.

Ronaldo (31), aliongeza kiasi cha Pauni 11 milioni na hivyo kufikia dau la Pauni 40 milioni kwa mwaka wakati Neymar wa Barcelona ameongeza mapato yake kuanzia Pauni 21 milioni hadi 27 milioni.

Wachezaji tisa wana pato la zaidi ya Pauni 15 milioni kwa mwaka akiwemo nahodha wa PSG, Thiago Silva anayeingiza Pauni 20 milioni kwa mwaka huku staa wa timu yake, Zlatan Ibrahimovic akiingiza Pauni 15.8 milioni.

Jumamosi, 30 Januari 2016

Samatta Lazima Ang'are Pale Grenk

Kwa fowadi hii ya Genk? Samatta labda arogwe

KWA mwanetu Mbwana Samatta tunayemjua na kwa Genk hii aliyokwenda,  labda alogwe. Lakini hakuna

Camargo

ADVERTISEMENT

KWA mwanetu Mbwana Samatta tunayemjua na kwa Genk hii aliyokwenda,  labda alogwe. Lakini hakuna kitakachomzuia kuingia kwenye kikosi cha kwanza baada ya jana Ijumaa jioni kusaini mkataba wa miaka minne ambao unaanzia 2016-2020 mwaka ambao Rais John Magufuli atakuwa anatimiza miaka mitano ya kuongoza nchi.

Samatta ameikuta Genk ina mastraika saba kutoka Uturuki, Jamaica, Ugiriki, Georgia na wazawa wa Ubelgiji.

Huyo straika wa Uturuki anaitwa Enes Unal ni mchezaji wa Manchester City ya England ambaye ameletwa Genk kwa mkopo wa misimu miwili huu ni msimu wake wa kwanza na amepachika bao moja tu katika mechi zaidi ya 10 alizocheza.

 Huyo wa Georgia ni jamaa mmoja mtata sana uwanjani anaitwa Nikolaos Karelis anatumia guu la kushoto, mpaka sasa amefunga bao moja tu.

Sasa kuna mashine zao mbili wanazoziaminia ijapokuwa kiuhalisia umri umewatupa. Mmoja anaitwa Igor Alberto Camargo ana miaka 32, huyu jamaa amefunga mabao matano tu katika mechi zote 23 alizocheza.

Ni Mbrazili aliyepewa uraia wa Ubelgiji. Hao wangapi? Staa mwingine ni kibabu pia ana miaka 34 wanamuita Thomas Buffel ni pande fulani la mtu amefunga mabao matatu. Huyo wa Jamaica anaitwa Leon Bailey ni bwana mdogo kuliko hata Samatta, yeye ana mabao matatu.

Hao mafowadi wengine wala hata usitake kuwajua utakuwa unapoteza muda wako tu. Ila kwa jinsi Samatta alivyopania lazima mtu aende benchi.Sikia sasa mastraika saba wa Genk kwa ujumla wao katika mechi zote 23 walizocheza wamefunga mabao 12. Buffel na Camargo wamefunga mabao manane kati ya hayo. Ukiangalia takwimu hizo za mabao unapata jibu la kwanini Kocha Mbelgiji, Peter Maes alimtaka Samatta kwa nguvu zote kuokoa kibarua chake. Genk ipo katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi ikiwa pointi 32, huku AA Gent wakiongoza msimamo kwa pointi 49.

Kwenye timu hiyo kuna Wakongomani wanne ambao wamezaliwa Ubelgiji wana uraia wa nchi mbalimbali. Wakongomani hao ni Derick Katuku Tshimanga ambaye ni beki wa kushoto anayetumia mguu wa kulia mwenye kilo 68 ana miaka 27.

Mwingine ni Christian Kabasele ambaye ni bonge la beki anatumia guu la kulia na kwa sasa amepachika mabao mawili kwenye ligi. Kuna Mkongo Mwingine anaitwa Neesken Kebano ni kiungo ana mabao matatu msimu huu.

Kuna Mnigeria anaitwa Onyinye Ndidi ni beki fulani mjanja mjanja mwenye bao moja. Yule Mghana Bennard Kumordzi ni beki. Wachezaji hao wameshazoea mazingira kwenye kikosi hicho na huenda wakawa msaada mkubwa kwa Mbwana Samatta ambaye jana Ijumaa alitaraji kufanyiwa vipimo vya afya pamoja na TP Mazembe kumalizana na Genk.

TP Mazembe jana ilikuwa kwenye mishemishe za kumalizana na Genk na kupokea dau lao la zaidi ya Sh.1.8 bilioni ambapo Simba wanasubiri mgao wao kutoka hapo. Klabu ya Genk  baada ya kushiriki Ligi ya Mabingwa mwaka 2012 iliwauza kipa wa sasa wa Chelsea, Thibaut Courtois na  Kevin De Bruyne ambaye pia alienda Chelsea kabla ya kutua Man City. Ilimuuza pia Christian Benteke kwa Aston Villa, sasa yuko Liverpool.

Gari La Wema Halina Vibali

Mama kijacho Wema Sepetu ‘Madam’

STORI: Mwandishi Wetu, Risasi Jumamosi

DAR ES SALAAM: Mama kijacho Wema Abraham Sepetu ‘Madam’ kwa mara nyingine ametengeneza kichwa cha habari, safari hii amewekwa chini ya ulinzi wa polisi kwa kosa la kuendesha gari aina ya Range Rover Evogue bila kuwa na vibali,Risasi Jumamosi lina ‘full’ stori.

Tukio hilo lililodumu kwa takriban saa tatu lilijiri Jumanne iliyopita maeneo ya Aficana, Mbezi Beach jijini Dar wakati mrembo huyo alipokuwa ‘kiguu na njia’ kwenda kwenye bethidei ya rafiki yake aliyefahamika kwa jina la Kibadude.

Gari lake likikaguliwa na maofisa wa TRA

NI LILE ALILODAI KUJIZAWADIA

Kwa mujibu wa chanzo makini kilichokuwepo eneo la tukio, gari hilo alilokamatwa nalo Madam ni lile alilojizawadia kwa mbwembwe nyingi mwishoni mwa mwaka jana katika siku yake ya kuzaliwa ambalo lina thamani ya shilingi milioni 200 za Kibongo.

“Nimepiga picha. Wamemtaiti hapa Mbezi Africana, naona maofisa wa TRA wanamhoji. Lina tatizo katika uhalali wa kuingia nchini. Hapa sasa naona wanaomhenyesha ile mbaya. Si kawaida.”

AMWAGA CHOZI

“Sasa namuona Madam machozi yanamtoka yenyewe… anahaha, mara aende huku mara kule. Nahisi so litakuwa limemkalia vibaya maana kila simu anayopiga hapati msaada,” kilinyetisha chanzo hicho.

Ukaguzi ukiendelea

TRA WABAINI FIGISUFIGISU

Gazeti hili lilizungumza na ofisa mmoja wa TRA ambaye alikuwepo kwenye tukio hilo aliyeomba hifadhi ya jina kwa kuwa si msemaji wa mamlaka hiyo aliweka wazi kuwa, walibaini figisufigisu katika gari hilo.

Range la Wema

“Hili gari ni moja kati ya magari ambayo yanaingia nchini kutokea nchi ya Msumbiji. Hata namba zake za usajili zinaonesha hivyo. Sasa huwa yanakatiwa vibali vya miezi mitatu au kulipiwa ushuru na kununuliwa. Liliingia nchini tangu mwaka jana.

“Tumekuta halina vibali maana vibali vya miezi mitatu vimeisha, tumemuuliza atoe nyaraka za gari, anasema zipo nyumbani, tukamwambia twende huko nyumbani ukazitoe, akabadili lugha, akasema anazo Steve (Nyerere). Inaonekana hili gari lina matatizo makubwa ya ushuru,” alisema ofisa huyo.

FIGISU NYINGINE

Kumbukumbu zinaonesha gari hilohilo la Wema ambalo alisema amejinunulia kwa fedha zake, ndilo alilodaiwa kununuliwa na mbunge machachari wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye aliwahi pia kutajwa kuwa ndiye baba kijacho wake kabla ya Idris Sultan kuibuka na kujinadi kuwa ndiye ‘mmiliki’ halali wa tumbo hilo.

KIGOGO SERIKALINI AMUOKOA

Paparazi wetu alimtafuta mtu wa karibu kabisa na Wema ambaye alieleza kuwa, Madam baada ya kuhaha kwa muda mrefu eneo hilo huku akiwa chini ya ulinzi wa polisi wenye bunduki, alipata wazo la kumpigia kigogo mmoja serikalini (jina tunalo) ambaye alimpa msaada kwa masharti.

“Alimpigia simu… (anataja jina la kigogo), akamweleza matatizo yaliyomkuta, naye akazungumza na maofisa wa TRA, wakakubaliana kwa masharti kwamba asilitumie gari hilo ndani ya wiki moja mpaka apeleke vibali vya gari hilo,” alisema mtu huyo wa karibu na Wema.

HUENDA LIKATAIFISHWA KAMA LA WOLPER

Kwa mujibu wa taratibu na sheria za TRA, endapo Wema atashindwa kutoa nyaraka muhimu za gari hilo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na  kutaifishwa kwa gari hilo kama ilivyomtokea mwigizaji Jacqueline Wolper ambaye mwaka 2014, gari lake aina ya BMW X6 lilikamatwa na kutaifishwa kwa kushindwa kulipia ushuru na kukosa vibali halali.

WEMA ASAKWA

Baada ya kupewa taarifa hizo, gazeti hili lilimtafuta Wema kwenye simu yake ya mkononi lakini muda wote iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu.

MENEJA WA WEMA ANENA

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, meneja wa msanii huyo, Martin Kadinda alisema yeye alisikia kwa watu kuhusu taarifa za Madam kukamatwa na gari hilo lakini alipomuuliza alimwambia si kweli, ni uzushi tu na hata gari hilo lipo nyumbani aende kuliona jambo ambalo alilifanya na kweli akajionea gari hilo.

“Ni uzushi tu. Nimeongea na Madam, akanihakikishia kwamba hamna kitu kama hicho. Nikaenda kulitazama gari, nikalikuta nyumbani kwake Ununio, shwari kabisa,” alisema Martin.

Gazeti ndugu na hili, Amani, toleo la Alhamisi iliyopita, ukurasa wa nyuma kulikuwa na habari yenye kichwa; Range la Wema layeyuka. Msingi wa habari hiyo ni taarifa kuwa, Wema haonekani akiwa na gari hilo licha ya kujinadi kuwa ni lake. Amekuwa akitumia kigari kidogo ‘ki-kirikuu’ kuendea kwenye shughuli zake.

Ilidaiwa kuwa, Wema alilipeleka gereji au yadi ya kuuzia magari, gari hilo hali iliyowafanya mapaparazi wa OFM kulisaka bila mafanikio huku ikielezwa kuwa, gari hilo si lake bali huwa anapepewa kwa muda kujiachia nalo.

Panga La JPM Laondoa Vichwa 152

Panga la JPM lachinja vichwa 152

Hakuna shaka kuwa Rais John Magufuli anatimiza ahadi yake ya kutumbua majipu aliyoitoa katika

Rais John Magufuli.

Dar es Salaam. Hakuna shaka kuwa Rais John Magufuli anatimiza ahadi yake ya kutumbua majipu aliyoitoa katika hotuba yake ya kwanza bungeni baada ya zaidi ya watumishi 152 wa Serikali kutimuliwa hata kabla ya siku 100 kutimia.

Hao ni watumishi waliotimuliwa kwa majina au vyeo vyao, lakini ukijumlisha na wengine waliosimamishwa au kufukuzwa kwa matamko bila kutajwa majina, idadi ni kubwa zaidi.

Watumishi hao wamesimamishwa na baadhi wamefukuzwa kazi kutokana na tuhuma mbalimbali za kukiuka Sheria ya Ununuzi wa Umma, Rais kutoridhishwa na utendaji wao, wizi kwenye taasisi zao, ukwepaji kodi, tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma na utovu wa nidhamu.

Hatua hizo ni utekelezaji wa ahadi ambazo Rais Magufuli alitoa kwenye hotuba yake ya kwanza bungeni Novemba 2, mwaka jana mjini Dodoma, alipoahidi kupambana na rushwa bila kigugumizi wala haya yoyote.

“Dawa ya jipu ni kulitumbua na mimi nimejipa kazi ya kuwa mtumbua jipu. Najua kutumbua jipu kuna maumivu lakini bahati mbaya halina dawa nyingine,” alisema.

Timuatimua hiyo, ambayo ilimgusa katibu mkuu wa wizara, wakurugenzi wa taasisi na watumishi waandamizi, ilifanywa pia na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na baadhi ya mawaziri wa JPM.

Hadi sasa, taasisi zilizopewa jukumu la kuwachunguza na kuwafikisha mahakamani watumishi walioonekana na matatizo, bado hazijatoa taarifa wala kuchukua hatua.

Akizungumzia kusimamishwa kazi kwa watumishi hao, mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais-Utumishi wa Umma, Florence Temba alisema iwapo Rais, Waziri Mkuu au Waziri ameagiza mtumishi asimamishwe kazi, huanza kuangaliwa wakati uchunguzi unafanyika.

Alisema iwapo kiongozi atasema mtumishi amefukuzwa kazi, ni dhahiri kuwa huyo ameondolewa kabisa katika ajira za Serikali.

“Hata hivyo, baadhi ya wanaosimamishwa huweza kuendelea kulipwa mishahara yao kulingana na mazingira ya kesi zao,” alisema.

Bosi wa Muhimbili

Hatua za kusimamisha na kutimua zilianza siku nne tu baada ya Rais kuapishwa, ambapo Novemba 9, 2015 alimsimamisha kazi kaimu mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Hussein Kidanto, na kuivunja bodi hiyo iliyokuwa na wajumbe 11.

Rished Bade

Rais Magufuli alimfukuza kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Rished Bade Novemba 27.

Bodi ya TPA

Desemba 7 , mwaka jana, Magufuli alivunja bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) pamoja na kutengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka, Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari, Profesa Joseph Msambichaka na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari, Awadh Massawe.

Bodi ya TPA ilikuwa na wajumbe wanane, ambao ni Dk Tulia Ackson, ambaye sasa ni Naibu Spika wa Bunge, Mussa Ally Nyamsingwa (Mhandisi wa Ujenzi), Donata Mugassa (mtaalamu wa ununuzi na mjumbe wa Bodi ya Posta), na Haruna Masebu (mkurugenzi mkuu mstaafu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura).

Wajumbe wengine ni Flavian Kinunda, Mhandisi Gema Modu, Dk Francis Michael na Crescentius Magori.

Pia, aliwasimamisha kazi wasimamizi wanane wa Bandari Kavu (ICD) ambao ni Happygod Naftari, Juma Zaar, Steven Naftari Mtui, Titi Ligalwike, Lydia Prosper Kimaro, Mkango Alli, John Elisante na James Kamwomwa.

Wengine ambao hawakuwamo kwenye ripoti hiyo ambao ni viongozi wa sekta zilizotoa ruhusa makontena kutoka ndani ya bandari lakini ni wahusika wakuu ni Shaban Mngazija aliyekuwa meneja mapato, Rajab Mdoe (mkurugenzi wa fedha na mkuu wa Bandari Kavu), Ibin Masoud (kaimu mkurugenzi wa fedha), Apolonia Mosha (meneja msaidizi wa Bandari-Fedha). Jumla ya waliotimuliwa TPA na TRA ni 47.

Dk Hoseah

Akiendelea na kasi yake ambayo ameipa jina “kutumbua majipu”, Desemba 16, 2015 Rais alitengua uteuzi nafasi nyeti ya mkurugenzi wa Takukuru, Dk Edward Hoseah. Rais alisema alichukua hatua hiyo baada ya kutoridhishwa na utendaji wa Takukuru chini ya mkurugenzi huyo.

Maofisa wengine wa taasisi hiyo walisimamishwa kazi kwa kukiuka maagizo yaliyohusu safari za nje. Waliosimamishwa kazi ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas, wakiwa watumishi waandamizi wa taasisi hiyo.

Bosi wa Rahco

Rais JPM alimsimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa kampuni hodhi ya rasilimali za Reli Tanzania (Rahco), Benhadard Tito Desemba 23, 2015 kwa kile kilichoelezwa ni “ukiukwaji mkubwa wa taratibu za ununuzi” katika mchakato wa utoaji wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kati. Pia alivunja bodi ya Rahco yenye wajumbe wanane na bodi ya TRL yenye wajumbe wanane pia.

Katibu tawala Mwanza

Akiendelea na kasi hiyo, Januari 15, alitengua uteuzi na kumfukuza kazi Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Faisal Issa kutokana na “utovu wa mkubwa wa nidhamu” aliounyesha katika kikao cha cha kamati ya ulinzi kilichofanyika mjini Mwanza.

Idara ya Uhamiaji

Rais Magufuli alimsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile na Kamishna wa Uhamiaji anayeshughulikia utawala na fedha, Piniel Mgonja Januari 21 ili kupisha uchunguzi baada ya kubaini dosari kadhaa kwenye ofisi hiyo.

Mkurugenzi Nida

Utumbuaji huo wa majipu haukushia hapo. Januari 25, Dk Magufuli alitengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu kutokana na matumizi yasiyoridhisha ya Sh179 bilioni.

Wengine waliosimamishwa Nida ni Joseph Makani ambaye ni mkurugenzi wa Tehama, Rahel Mapande (ofisa ugavi mkuu), Sabrina Nyoni (mkurugenzi wa sheria) na George Ntalima, ofisa usafirishaji.

Pia, aliwarudisha nyumbani mabalozi wawili, Dk Batilda Buriani aliyekuwa Japan, Dk James Msekela (Roma, Italia). Pia, Peter Kallaghe (Uingereza) na kurejeshwa Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano, Kikanda na Kimataifa.

Waziri Mkuu

Wakati Rais Magufuli akitimua watumishi hao wa umma, Novemba 27, mwaka jana, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimsimamisha kazi Kamishna wa Kodi na Forodha wa TRA, Tiagi Masamaki, Habibu Mponezya wa kitengo cha huduma kwa wateja, Haruni Mpande na Hamis Ali wa kitengo cha Tehama na Eliachi Mrema wa Bandari Kavu. (ICD).

Baadaye Novemba 29, Majaliwa aliwafukuza wafanyakazi watatu wa TRA, Anangisye Mtafya, Nsajigwa Mwandengele na Robert Nyoni.

Kigoma

Majaliwa aliwasimamisha watumishi tisa wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Januari 8 kwa tuhuma za kuingia mikataba mibovu isiyokuwa na tija na kuisababishia manispaa kupoteza mapato. Pia wanatuhumiwa kulipa fidia batili na kuuza mali za halmashauri kinyume cha sheria.

Ruvuma

Kadhalika, akiwa mkoani Ruvuma Januari 8, Majaliwa alimsimamisha kazi meneja uendeshaji wa kiwanda cha kusindika tumbaku (Sontop), Paul Balegwa akidaiwa kushiriki kwa namna moja au nyingine kufanya ubadhirifu wa fedha za wakulima na hivyo kiwanda hicho kusitisha uzalishaji kwa zaidi ya miaka 18 iliyopita.

Mawaziri

George Simbachawene (Tamisemi) alimsimamisha kazi mtendaji mkuu mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (DART), Asteria Mlambo.

Waziri huyo pia alitoa agizo la kusimamishwa kwa ofisa biashara wa Manispaa ya Ilala, Dennis Mrema. Hali kadhalika, Mkurugenzi wa Manispaa za Kigoma, Mhandisi Boniface Nyambele na mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda, Suleiman Lukanga.

Simbachawene pia aliwasimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Dodoma, Augustino Kalinga na wenzake kaimu ofisa biashara wa manispaa hiyo, Elias Kamara na Donatila Vedasto kwa kosa la kusababisha urasimu katika utoaji wa leseni za biashara.

Profesa Makame Mbarawa (Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano), amewasimamisha kazi wafanyakazi 15 wa Mamlaka ya Bandari kwa tuhuma za upotevu wa Sh48 bilioni.

Wizara pia iliwasimamisha wakuu wanne wa idara wa kampuni ya huduma za meli (Marine) kwa tuhuma ya ubadhirifu wa zaidi ya Sh600 milioni.

Profesa Jumanne Magembe (Maliasili na Utalii), amemsimamisha kazi mkurugenzi wa mipango na matumizi endelevu ya rasilimali za misitu wa wakala wa misitu nchini, Mohammed Kilongo na maofisa wa misitu wa mikoa yote nchini.

Mwigulu Nchemba (Kilimo, Mifugo na Uvuvi), amemtimua mkuu wa mnada wa mifugo wa Pugu na watumishi walioshiriki kuiba ushuru wa Serikali.

Pia aliagiza viongozi tisa wa vyama vya ushirika vya Mfyome, Magubike, Kiwemu, Kitai, Mhanga na Kampuni ya Umoja wa Wakulima wa Tumbaku Iringa (ITCOJE Ltd), wakabidhi ofisi zao kutokana na tuhuma za kutapeli trekta za mkopo.

Ummy Mwalimu (Afya), amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Diwani Msemo.

Jenista Mhagama (Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), alimtimua mkandarasi wa mfereji wa Buguruni kwa Mnyamani.

Simiyu

Januari 29, Rais John Magufuli aliwafukuza kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Bariadi, Erica Mussika kwa shindwa kusimamia mradi mkubwa wa barabara wa Sh9.192 bilioni, uliofanikishwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia na amemfukuza kazi Mhandisi wa ujenzi, Ruben Muyungi.

Maoni ya wasomi

Akizungumzia hatua hizo, mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Hamad Salim alisema anapata shaka na aina hiyo ya utendaji.

“Labda kwa Rais ambaye huenda akawa na mkono mrefu wa kupata taarifa kuhusu watendaji anaowachukulia hatua, ila kwa hao wengine napata shaka,” alisema.

Salim alisema anachokiona kwa mawaziri ni ushabiki wa kuiga staili ya utendaji wa Rais Magufuli, ili waonekana wanafanya kazi.

Naye, Dk Benson Bana alisema maamuzi hayo yana matokeo ambayo ni ya sura mbili, hasi na chanya.

Dk Bana, ambaye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alisema kufanya hivyo kutasababisha watumishi wa umma wafanye kazi kwa woga.

Alisisitiza kuwa kwa wale wanaosimamishwa kupisha uchunguzi, unapomalizika na mtumishi akibainika hana hatia, basi atangazwe kuwa amerejeshwa kazini kuliko mambo kufanyika kimyakimya.

“Kwa sasa wafanyakazi wanafanya kazi wakiwa na hofu kwamba huenda waziri atatokea itakuwaje, “ alisema Bana.

Akizungumzia matokeo chanya, alisema hatua ya kuwajibishwa watendaji hao, imerejesha utendaji mzuri katika ofisi za umma kwa sababu kuna baadhi zilikuwa zimekithiri ufisadi, rushwa na uzembe.

-

Balozi Amina:Bado nautaka Uraisi

Balozi Amina: Bado nautaka urais

Amina Salum Ali, ambaye alishika nafasi ya pili kwenye mbio za urais ndani ya CCM, amesema ndoto

Balozi Amina Salum Ali .

Amina Salum Ali, ambaye alishika nafasi ya pili kwenye mbio za urais ndani ya CCM, amesema ndoto yake ya kushika nafasi hiyo ya juu katika siasa nchini, haijafa.

Amina, ambaye alikuwa balozi wa Afrika kwenye Umoja wa Mataifa, alisema hayo kwenye mahojiano maalum na Mwananchi yaliyofanyika mapema wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

Balozi Amina alichomoza kwenye mbio za urais ndani ya CCM baada ya kuingia tano bora, akiwa pamoja na John Magufuli, Asha Rose Migiro, January Makamba na Bernard Membe na baadaye kuingia tatu bora kwa ajili ya kupigiwa kura na Mkutano Mkuu wa chama hicho ambao ulimchagua Magufuli kugombea urais.

Lakini Balozi Amina, ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 59, anasema hilo halijaondoa ndoto yake ya kuingia Ikulu.

“Sikushiriki Uchaguzi Mkuu mwaka jana kwa ajili ya kujaribu bahati yangu, bali nilikuwa na nia ya dhati ya kushinda urais na kuwatumikia wananchi,” alisema Balozi Amina.

“Sikushiriki Uchaguzi Mkuu mwaka jana kwa ajili ya kujaribu bahati yangu, bali nilikuwa na nia ya dhati ya kushinda urais na kuwatumikia wananchi,” alisema Balozi Amina.

“Nilitamani kweli niwe rais na niseme tu kwamba kwa kweli ndoto yangu hiyo haijafa, ingawa jambo hilo sasa litategemea muda, uhai, afya na mazingira yatakayojitokeza baada ya Rais Magufuli kumaliza muhula wake wa uongozi,” alisema.

Kwa mujibu wa utaratibu wa CCM, kada anayechaguliwa kuwa Rais hupitishwa tena kugombea urais baada ya kipindi chake cha miaka mitano kumalizika ili aongoze nchi kwa vipindi viwili.

Balozi Amina anasema safari yake ya kuelekea Ikulu ilikumbwa na vikwazo viwili, ambavyo alivitaja kuwa ni Watanzania kutokuwa tayari kuongozwa na mwanamke na pia mchakato wa uchaguzi kutawaliwa na wenye fedha.

Alisema bado jamii haijawa tayari kuamini kuwa mwanamke anaweza kuwa kiongozi wa juu wa ngazi kama ya urais, lakini anasema jitihada za CCM kwenye uchaguzi uliopita kumkubali mwanamke zinaweza kubadilisha mtazamo wa jamii.

“Mimi naona tatizo hilo limesababishwa na mambo mengi. Inaweza ikawa tatizo la elimu kwamba watu bado hawajaelewa vya kutosha kwamba mwanamke anaweza,” alisema.

“Lakini pia hili ni suala la mila na desturi. Kuna baadhi ya maeneo nchini mwanamke hachukuliwi kama ana mchango wowote katika maendeleo ya jamii. Lakini ninavyoona hali hii itakwisha na tumeanza kuimaliza baada ya kumpata Makamu wa Rais Mwanamke.”

Amina alibainisha kuwa mawazo kwamba mwanamke hawezi kuwa kiongozi ni potofu, ingawa na yametokana pia na ukweli kwamba baadhi ya wanawake hawajajitambua vya kutosha.

“Kuna uwezekano Tanzania ikaongozwa na mwanamke na watu waondoe mawazo kuwa mwanamke hafai kuwa kiongozi. Wanawake wana uwezo mzuri, ila wanachohitaji kutoka kwa jamii ni kuwaamini tu,” alisema.

Jambo jingine ni mchakato wa uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kupitia CCM, na hasa nafasi ya Urais.

Alisema utaratibu unaotumika sasa kuanzia uchukuaji wa fomu mpaka uteuzi, unatengeneza makundi ya walionacho na wasionacho ndani ya chama hicho na hivyo kuwafanya baadhi ya wanachama kushindwa kukabiliana na ushindani.

“Chama kiimarishe process (mchakato) za kutafuta wadhamini, kiangalie upya mfumo na ikiwezekana turudi kwenye mfumo wa zamani wa kamati ya utendaji kuwachuja wagombea,” alisema Kuhusu mkakati wake endapo angepitishwa na baadaye kuchaguliwa kuwa Rais, Balozi Amina alisema alitaka wananchi wanufaike na kukua kwa uchumi.

“Nilitaka nitafsiri kukua kwa uchumi mifukoni mwa wananchi,” alisema.

Amina alisema haina maana kueleza kuwa uchumi wa nchi unakua wakati Watanzania bado wanaishi maisha ya umaskini na hicho ndicho kilikuwa kilio chake.

Alieleza wakati sera zikielekeza kuhusu viwanda na kilimo, dira yake ingekuwa kusimamia uboreshaji wa mazao ya kilimo na viwandani ili yaongezwe ubora kabla ya kuuzwa, kitu ambacho alisema kingesaidia kuongeza ajira kwa vijana.

“Nilitamani kuona kama tunazalisha mazao ya kilimo, tuyasindike kwanza kabla ya kuuza. Na bidhaa za viwandani hivyo hivyo ili tuongeze ubora na kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaongeza ajira kwa vijana,” alisema.

Pia, alisema angesimamia ukusanyaji wa kodi kama inavyofanywa sasa na Serikali ya Rais Magufuli, lakini yeye asingeishia kusimamia makusanyo ya kodi inayoingia kupitia bandari pekee, bali angetafuta vyanzo mbadala vya uhakika vya kuongeza mapato ya Serikali.

“Kukusanya mapato bandarini ni sawa, lakini bandari si chanzo cha mapato cha kutegemea sana, kwani bidhaa zinaingia bandarini kama dunia haijachafuka. Ikitokea machafuko kwenye nchi ambazo zinatumia bandari zetu hatuwezi kupata mizigo ya kuitoza kodi. Kumbe ningetafuta vyanzo vingine vya uhakika zaidi vya mapato,” alisema.

Uchaguzi Mkuu ulikuwa huru na wa haki

Kuhusu tathmini ya uchaguzi, Balozi Amina alisema ulikuwa huru kwa vigezo vyote vya ndani na nje ya nchi.

“Uchaguzi ulikuwa huru na wa haki na hata Umoja wa Mataifa unatambua hilo. Pia waangalizi mbalimbali wa kimataifa walieleza kuwa uchaguzi ule haukuwa na shida,” alisema.

-

Alhamisi, 28 Januari 2016

Bungeni Ni Balaa tu

Ni mzobemzobe bungeni

Polisi 35 jana walitumika kuwatoa ukumbini wabunge kutoka vyama vya upinzani baada ya vurugu

Makachero na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge baada ya kuitwa na Mwenyekiti Andrew Chenge ili kuwatoa kwa nguvu wabunge wa upinzani kwa kukaidi amri ya kuwataka waende nje jana. Picha na Edwin Mjwahuzi

Dodoma. Polisi 35 jana walitumika kuwatoa ukumbini wabunge kutoka vyama vya upinzani baada ya vurugu kutokea ndani ya chombo hicho cha kutunga sheria kutokana na tangazo la uamuzi wa Shirika la Utangazaji (TBC) kupunguza matangazo ya moja kwa moja ya shughuli za Bunge.

Wabunge wa upinzani walitolewa ukumbini wakiwa wamebebwa juu juu au mzobemzobe, wengine wakiwa wamechaniwa nguo na wengine kurushiana makonde na polisi katika tukio lililoweka taswira ya kwanza ya aina yake tangu kurejeshwa kwa siasa za vyama vingi mwaka 1992.

Waandishi wa habari waliokuwa ndani ya ukumbi wa Bunge, walizuiwa kwanza kuchukua picha za matukio yaliyokuwa yakiendelea ukumbini hapo, na baadaye kuondolewa na kupelekwa kwenye chumba kingine na hivyo kushindwa kufanya vizuri kazi yao ya kuchukua habari.

Kabla ya purukushani hizo kuanza, asubuhi kituo cha televisheni cha TBC1 kilikatisha matangazo yake ya moja kwa moja mara baada ya Waziri wa Habari, Nape Nnauye kutangaza uamuzi wa chombo hicho kupunguza matangazo ya moja kwa moja ya shughuli za Bunge. Baadaye kituo cha televisheni cha Star TV nacho kikakatisha matangazo na hivyo kubakia Azam TV tu.

Lakini jioni, wakati mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge akijiandaa kutangaza uamuzi wa kuwaondoa ukumbini wabunge wa Ukawa, mtangazaji wa Azam TV naye akatangaza kuwa kituo hicho kinakatisha matangazo hayo ya moja kwa moja.

Dalili za vurugu hizo zilianza kuonekana asubuhi wakati wabunge wa upinzani walipopinga kujadili hotuba ya Rais John Magufuli aliyoitoa Novemba 20 wakati TBC ikiwa imezima matangazo ya moja kwa moja, wakidai wananchi wana haki ya kusikia kinachojadiliwa.

Hoja hiyo ilisababisha Chenge kuahirisha shughuli za Bunge kuipa nafasi Kamati ya Uongozi kujadili na kutolea uamuzi hoja ya mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ya kupinga mjadala wa hotuba ya Rais kutorushwa moja kwa moja na televisheni ya taifa.

Chenge aliahirisha shughuli hizo hadi saa 10:00 jioni wakati vurugu zilipoibuka.

Baada ya mvutano wa dakika 35 kati ya Chenge na wabunge wa upinzani kuhusu kanuni, vurugu hizo zililipuka saa 10:50 jioni.

Askari hao walitumia takriban dakika 25 kuwatoa wabunge hao ukumbini baada ya kuanza mzobemzobe huo saa 10:50 jioni na kuumaliza saa 11:15 jioni.

Wabunge hao walizua sintofahamu baada ya Chenge kueleza uamuzi wa Kamati ya Uongozi iliyokutana jana mchana kujadili hoja iliyotolewa asubuhi na Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo, Kigoma Mjini), kupinga kusitishwa kurushwa kwa matangazo hayo, kauli ambayo ilisababisha mwenyekiti huyo kuahirisha kikao hicho mpaka saa 10:00 jioni kutokana na shinikizo la wabunge wa upinzani.

Wakati wabunge wakibebwa juu juu na askari hao, ofisa habari wa Bunge, Owen Mwandumbya aliwataka waandishi wote wa habari kutofanya chochote, ikiwa pamoja na kupiga picha, na kuwataka watoke nje ya ukumbi wa Bunge hadi kwenye eneo maalumu lililokuwa na ulinzi wa askari.

Akieleza uamuzi wa kamati ya uongozi, Chenge alisema: “Kwanza kamati imesema mwenyekiti wa Bunge alikuwa sahihi kuahirisha Bunge, pili hakuna haki iliyovunjwa, tatu kamati imeagiza mjadala wa hotuba ya rais uendelee na nne endapo kuna mbunge hajaridhika ni haki yake  kutumia kanuni ya 5 (4) ya kanuni za Bunge ili kuwasilisha malalamiko yake kwa Katibu wa Bunge”.

Uamuzi huo uliwanyanyua wabunge wa upinzani. Safari hii mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliomba mwongozo wa suala hilo, akisema kuwa lilipaswa kutolewa uamuzi na mwenyekiti wa Bunge au Spika na  si kamati ya uongozi.

Katika hoja yake ya pili, Lissu alisema suala hilo ni la kikanuni na lilipaswa kutolewa ufafanuzi na Kamati ya Kanuni na si Kamati ya Uongozi, jambo ambalo lilipingwa na Chenge aliyesema kuwa kamati ya uongozi inaweza kujadili masuala ya kanuni.

Majibu ya Chenge yaliwanyanyua wabunge wote wa upinzani, huku Pauline Gekul (Babati Mjini) na John Heche (Tarime Vijijini) wakiomba mwongozo ambao Chenge alijibu kwa kurejea uamuzi wa Kamati ya Uongozi.

 Kutokana na wabunge hao kugoma kukaa huku wakipiga kelele, kujibiwa na wabunge wa CCM waliokuwa wakishangilia kwa mtindo wa kupiga meza, saa 10:50 jioni Chenge aliamuru askari wa Bunge kuwatoa wabunge hao.

Kabla ya uamuzi huo, Chenge aliamuru Lissu, Ester Bulaya (Bunda), Gekul na Godbles Lema (Arusha Mjini) kutoka nje ya ukumbi wa Bunge kwa maelezo kuwa ndio walikuwa vinara wa vurugu hizo.

Hata hivyo, wabunge hao waligoma huku Lema akisimama na kuvua koti na tai, akisema kuwa hakuwa akizungumza chochote.

Baada ya Chenge kutoka nje ya ukumbi wa Bunge, polisi wanane waliingia kuwatoa wabunge hao bila mafanikio, na kulazimika kuita polisi 18 waliokuwa wamevaa sare pamoja na wengine nane waliovaa kiraia.

Licha ya wingi wa askari hao ambao walizunguka eneo wanalokaa wabunge wa upinzani, walishindwa kuwatoa na kulazimika kuwaita askari tisa wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kuongeza nguvu.

Wabunge kadhaa walitolewa ndani ya ukumbi wa Bunge huku wakiwa wamebebwa juu juu na kuchaniwa nguo zao, kusababisha baadhi yao kurushiana makonde na askari hao.

Baada ya askari hao kufanikiwa kuwatoa nje, wabunge waliosalia ambao ni kutoka CCM waliendelea kujadili hotuba ya Rais, huku waandishi wa habari nao wakitakiwa kurejea ukumbini.

 

Kauli ya Ukawa

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kwenye kikao cha Kamati ya Uongozi, Serikali ilibadili mjadala kutoka gharama za kurusha matangazo hayo na kuibuka na madai kuwa watumishi wa Serikali hawafanyi kazi kwa sababu ya kuangalia matangazo ya Bunge.

“Pia Serikali ilileta hoja kuwa wakati wa mchana wananchi hawatazami televisheni na usiku ndio wanakuwa na muda zaidi. Sisi tulipinga hoja hizo kwa kutambua kuwa huo ni mkakati maalumu wa Serikali na ulianza tangu wakati wa kampeni, sasa umefikia hatua ya kufungia vyombo vya habari,” alisema Mbowe.

“Walianza siku nyingi na hata kufikia hatua ya kuzuia vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara. Uamuzi huu utawafanya wananchi kutosikiliza taarifa za Serikali.”

Alisema walirejea kwenye kikao cha Bunge jioni kwa nia ya kupinga uamuzi wa Serikali kuzuia matangazo hayo kwa lengo la kuijulisha dunia juu ya kinachofanywa na Serikali ya CCM.

“Watu wanafukuzwa kazi bila kufuata taratibu, mfano ni mabalozi waliotakiwa kurudi nyumbani haraka. Huku ni kujenga misingi ya udikteta katika taifa. Mawaziri nao wanafukuza watu hovyo, wakuu wa wilaya ya mikoa nao, halafu  sisi tunasema ni majipu?” alihoji Mbowe.

“Tunalaani Serikali ya Magufuli kwa kutozingatia uhuru wa wananchi kupata habari, uhuru wa Bunge kusikilizwa. Tutapaza sauti ndani na nje ya Bunge. Hatuwezi kuruhusu mambo haya kuonekana ni utaratibu wa kawaida.”

Alisema kuna taarifa kuwa Serikali inahofia kujadiliwa kwa suala la Zanzibar, yaliyotokea katika Uchaguzi Mkuu,“Tutaonyesha upande wa pili wa Serikali ya Magufuli,” alisema.

 Alisema vyombo vya dola vinatumika kuziba haki na uhuru wa wananchi, kama majeshi yanavyotumika kudhibiti wananchi baada yakufutwa kwa uchaguzi Zanzibar.

“Sasa tumeonyeshwa kuwa Bunge ni pamoja na FFU, polisi na mbwa. Tulichokitaka ni mjadala wa kutetea wananchi kupata habari. Chenge kakimbia kiti na kuacha Bunge kuongozwa na askari,” alisema Mbowe.

Alipoulizwa kama watashiriki katika kikao cha Bunge cha leo, Mbowe alisema: “Kesho (leo) tutaingia bungeni. Tambueni kuwa hata nyinyi (waandishi) mlifukuzwa. Ipo siku mtafukuzwa kabisa maana Serikali haitaki kuambiwa ukweli. Serikali ikifanya jema tutawapongeza, isipofanya jema tutasema.”

Alisema kuna wabunge wameumizwa kwa kipigo, kuibiwa saa, pochi na simu.

“Bunge kuendelea ni unafiki wa wabunge wa CCM. Asubuhi wakati tunashinikiza Bunge lijadili hoja hii, wabunge wa CCM walituandikia vikaratasi kutuunga mkono ila jioni wametugeuka,” alisema.

Baadhi ya waandishi waliojiwa na Mwananchi baada ya sakata hilo walisema inasikitisha kuona wanafanyiwa vitendo hivyo.

 

Kauli za wanahabari

Mwandishi wa gazeti la Mtanzania, Elias Msuya alisema: “Ni jambo la kusikitisha maana tumepewa vitambulisho kwa ajili ya kuandika habari za Bunge, lakini leo hii tunafukuzwa. Imeniuma sana.”

 Kwa upande wake mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, Ibrahim Yamola ambaye aliporwa simu yake na askari baada ya kupiga picha, alisema: “Ni tukio la kusikitisha, ni kama tulizuiwa kufanya kazi yetu.”

Wakati huo huo, msemaji wa Bunge, Owen Mwandumbya amesema kuwa waandishi wa habari saba watarudishwa na hawataruhusiwa kuripoti habari za Bunge kwa kile kilichoelezwa kukiuka kanuni na taratibu za Bunge.

Hata hivyo, hakuwataja moja kwa moja waandishi hao wa habari na kusema sababu kubwa ni kugoma kutii maagizo ya kutotakiwa kwenye baadhi ya maeneo ya Bunge na zaidi wakati wa vurugu hizo.     

-

Jumatano, 27 Januari 2016

Man City uso kwa uso na Liverpool Fainali za Capital one

ImageGetty

Man City imekua timu ya pili kufuzu fainali ya mchezo wa kombe la Capital baada ya kuichapa Everton kwa mabao 3-1.

Everton ndio walikua wa kwanza kuzifumani nyavu za Man city baada ya kiungo Ross Barkley kuifungia timu yake bao la kuongoza katika dakika ya 18 ya mchezo.

Kiungo wa kibrazl Fernandinho akasawazisha bao hilo kwa shuti kali baada ya kutoka piga nikupige kwenye goli la everton katika dakika ya 25.

Kevin De Bruyne akaongeza bao la pili baada ya kunganisha krosi ya kutoaka upande wa kushoto iliyopiga na Raheem Sterling, kina Sergio Aguero kun, akahitimisha kazi kwa bao la tatu.

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Goodson Park Everton walishindwa kwa ushindi wa mabao 2-1.

Man City watachuana na Liverpool katika mchezo wa fainali utaofanyika februari 28 katika dimba la la Wembley.

Toyota Yaongoza kwa Mauzo Duniani

ImageReutersImageKampuni ya magari ya Toyota

Toyota inaendelea kuongoza kama kampuni inayotengeza magari kwa mwaka wa nne mfululizo.

Kampuni hiyo iliuza magari milioni 10.15 kwa jumla mwaka 2015 na kuvunja rekodi ya matarajio ya wengi.

Kampuni ya Ujerumani ya Volkswagen imekuwa ya pili ikiwa imeuza magari milioni 9.93,ikifuatiwa na General Motors kutoka Marekani iliouza magari milioni 9.8.

Volkswagen ilikuwa inaongoza nusu ya mwaka wa 2015 kabla ya kashfa ya magari yake kutoa moshi mchafu kupunguza mauzo yake.

Biashara katika masoko makubwa kama vile Marekani na Japan na masoko yanayoinuka imepungua kutokana na kuanguka kwa uchumi duniani.

ImageAFPImageToyota

Mwaka 2014,Toyota iliibuka kidedea kwa kuuza magari milioni 10.23.

Kampuni hiyo imepata sifa kwa magari yake aina ya Prius hybrid,Camry,Corolla Sedan na Lexus.

Mauzo Ya Simu Za iphone Yapungua Duniani

ImageGettyImageMauzo ya simu ya Iphone yapungua

Kampuni kubwa ya teknolojia ya Apple imeripoti kupungua kwa mauzo ya simu za iPhone katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho mwaka uliopita.

Kampuni hiyo iliuza simu milioni 75 mwaka uliopita ikiwa ni mauzo ya chini zaidi tangu mwaka 2007.

Hii ni kutokana na kuyumba kwa uchumi wa China.

Hata hivyo faida ya kampuni ya Apple iliongezeka katika kipindi hicho kwa zaidi ya dola bilioni 18.

Mhariri wa masuala ya Teknolojia katika mtandao wa CNET Ian Sherr, amesema huenda soko la simu za mkononi limefurika.

Chelsea na Westbrom Watozwa faini

ImageRex FeatureImageChelsea na West Brom watozwa faini

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza, Chelsea na West Brom wametozwa faini kwa utovu wa nidhamu uwanjani katika mechi iliyozongwa na ubishi mwezi uliopita.

Shirikisho la soka nchini Uingereza FA limeitoza Chelsea faini ya pauni £65,000.

West Brom kwa upande wake imepigwa faiani ya pauni £35,000.

ImageMabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza, Chelsea na West Brom wametozwa faini kwa utovu wa nidhamu

Mshambulizi mbishi wa Chelsea Diego Costa alihusika katika mengi ya makabiliano hayo uwanjani.

Mhispania huyo alishambuliana na kiungo cha kati wa West Brom, Claudio Yacob baada ya kuangushwa.

West Brom walijifurukuta kutoka nyuma na kutoka sare na wenyeji wao Stamford Bridge.

ImageGettyImageCosta alihusika katika mengi ya makabiliano hayo uwanjani.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari FA inasema kuwa timu zote mbili zilishindwa kudhibiti wachezaji wake.

Yacob, ambaye alikuwa keshaoneshwa kadi ya njano kwa kumuangusha Costa, aliondolewa uwanjani na kocha Tony Pulis.

Siku chache baadaye kocha wa muda wa Chelsea Guus Hiddink alielezea kutoridhika na uamuzi wa refarii Anthony Taylor, akisema kuwa alipaswa kumuonesha kadi nyekundu Yacob

Ramires Asajiliwa China


I
Ramires
ImageRamires alijiunga na Chelsea kutoka Benfica 2010
Kiungo wa kati wa Chelsea Ramires amekamilisha kuhamia klabu ya Uchina Jiangsu Suning.
Ripoti zinasema Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 28 amenunuliwa £25m.
Alitia saini mkataba mpya wa miaka minne Chelsea Oktoba mwaka uliopita lakini ameanza mechi saba pekee za Ligi ya Premia msimu huu.
Jiangsu walimaliza nambari tisa katika ligi kuu ya Uchina 2015 na mkufunzi wao ni difenda wa zamani wa Chelsea Dan Petrescu.
Ramires alisaidia Blues kushinda Ligi ya Premia, Kombe la FA, Kombe la Ligi, Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na Uropa Ligi.
ImageVIPCOMM
Kwa jumla, alichezea Chelsea mechi 251, na kuwafungia mabao 34 kipindi alichokaa Stamford Bridge.
Ramires alinunuliwa £17m na Chelsea kutoka Benfica mwaka 2010

Azikwa Na Mali Zake Zote

Azikwa na kreti za bia na soda Kahama

Wakati serikali ikipigia kelele kukemea imani za kishirikina, wilayani Kahama bado ni kitendawili

TWEET

Kahama. Wakati serikali ikipigia kelele kukemea imani za kishirikina, wilayani Kahama bado ni kitendawili baada ya mkazi mmoja wa Kijiji cha Mwamande, Kata ya Mwanase katika Halmashauri ya Msalala kufariki na baadaye wanakijiji kumzika na mali zake zote yakiwemo makreti ya bia na soda aliyokuwa akiyatumia kwenye biashara yake ya baa.

Tukio hilo limetokea  jana katika kijiji hicho baada ya mwanakijiji huyo, Mahushi Lutaja kufariki na baadaye familia yake kupitisha maadhimio ya kumzika na mali zake zote kwa imani ya kwamba kifo chake kimetokana na kurogwa na wao kuhofia kwamba wakibaki na mali zake nao watakumbwa na mauti.

Kwa mujibu wa diwani wa Kata ya Mwanase, Samson Masanja, Lutaja baada ya kifo chake alizikwa na baisikeli moja vitanda vinne na magodolo yake pamoja na masanduku ya nguo zake zote na vitu vingine vidogovidogo alivyokuwa akivitumia

Pia Masanja alisema, Lutaja alizikwa na makreti ya bia na soda ambayo kabla ya kifo chake alikuwa akiyatumia kwenye biashara yake ya kuuza vinywaji kwenye kijiji hicho cha Mwamande ambapo  tukio hilo limehusishwa na imani za kishirikina

Wakati akiugua ndugu zake waliamini kwamba ugonjwa huo uliopelekea kifo chake ulitokana na kurogwa hivyo familia yake iliingiwa na hofu hiyo hasa kutokana na kuwepo madai ya waganga wa jadi kuamini kwamba ndugu yao alirogwa

 

Bunge Kutorushwa Live Kwazua Kizazaa

Mwenyekiti wa kikao cha Bunge Andrew Chenge.

Mwenyekiti wa kikao cha Bunge Andrew Chenge ameahirisha kikao cha Bunge kilichokuwa kikiendelea leo mjini Dodoma baada ya kutokea sintofahamu.

Chenge amefikia uamuzi huo kutokana na kuibuka kwa mjadala mkali kutoka kwa Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kulitaka bunge liahirishe kikao cha kujadili hotuba ya Rais Dk. Magufuli ili wabunge wajadili hoja ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye.

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.

Hoja ya Waziri Nape Nnauye ilikuwa ni kwamba Television ya Taifa (TBC) haitarusha matangazo ya moja kwa moja ya bunge (live) bali kutakuwa na kipindi maalumu kitakachoitwa leo katika Bunge litakachokuwa kikirekodiwa na kuonyeshwa usiku.

Hoja hiyo imezua mjadala mkali na kumfanya mwenyekiti wa Bunge kuahirisha kikao cha bunge kwa muda wa saa moja ili kikao cha kamati ya bunge kikakae na baadaye waje na njia muafaka ya kuweza kutatua jambo hilo.

Sumaye na Lowassa Kuendelea Kupata Pensheni

‘Lowassa, Sumaye watandelea kupata pensheni’

Serikali imesema leo kuwa mawaziri wakuu waliokihama Chama cha Mapinduzi (CCM) wataendelea

Edward Lowassa na Fredrick Sumaye 

Serikali imesema leo kuwa mawaziri wakuu waliokihama Chama cha Mapinduzi (CCM) wataendelea kulipwa pensheni zao kwa mujibu wa sheria ya nchi.

Mawaziri wakuu hao; Fredrick Sumaye na Edward Lowassa walihama CCM na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Mandeleo (Chadema)na badaye Lowassa aligombea urais chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Akijibu maswali ya baadhi ya wabunge waliohoji endapo watu waliokuwa katika nyadhifa hizo wanaweza kuzuiwa kuchukua pensheni zao kwa kuhamia upinzani, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Utumishi wa Umma, Angellah Kairuki amesema sheria haizuii kwa kuwa kuhama chama ni haki ya kikatiba.

Akinukuu Sheria ya mwaka 1999 pamoja na ile ya mwaka 2005 ya Utumishi wa Umma, Kairuki amesema waliokuwa viongozi katika nyadhifa hizo wana haki ya kuendelea kupata stahiki hizo kisheria.

Hata hivyo ameonya kuwa, wanapaswa kuheshimu sheria ya nchi inayowazuia kutoa siri za nchi wakati wakiwa katika nyadhifa zao.

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji, amesema uchumi ukiimarika utaisaidia serikali kuwalipa wastaafu pensheni itakayokidhi mahitaji yao. 

Jumanne, 26 Januari 2016

Meli Yenye Maktaba Yawasili Jijini Dar-es-salaam

Meli yenye maktaba yatia nanga Bandarini Dar es Salaam

Meli ambayo imebeba maelfu ya vitabu, ambayo huhudumu kama maktaba, imetia nanga bandarini Dar es Salaam.Meli hiyo ina zaidi ya vitabu 5,000 pamoja na video.

Aubameyang, "Yaya Toure Aliniudhi Sana Sikuile"

ImageGettyImageAubameyang akituzwa tuzo la mchezaji bora Afrika 2016

Pierre Emerick Aubameyang amesema kuwa alihisi uchungu baada ya Yaya Toure kusema kwamba 'sio heshima' kwa yeye kutunukiwa tuzo ya mchezaji bora barani Afrika mwaka uliopita.

Mchezaji huyo wa Manchester City alisema kwamba hatua hiyo ilileta aibu kwa bara la Afrika,huku mchezaji wa Swansea Andrew Ayew pia akihoji hatua hiyo.

Toure wa taifa la Ivory Coast na Ayew wa Ghana walifika katika fainali za kombe la Afrika huku Gabon ikitolewa mapema.

ImageGettyImageYaya Toure wa Ivory Coast

''Nilisikia uchungu sana na kile kilichosemwa'',alisema mshambuliaji huyo wa Borussia Dortmund Aubameyang.''Ni aibu''.

Katika kura iliopigwa na makocha na wakurugenzi wa kiufundi katika mataifa ya shirikisho la CAF,Aubameyang alipata kura 143,Toure akipata 136 huku Ayew akijipatia 112.

Toure,ambaye alitangazwa kuwa mchezaji bora wa 2015,alishinda tuzo hiyo kwa kipindi cha miaka minne iliopita mfululizo.

ImageGettyImageAndrew Ayew kulia

''Tuzo hiyo ni ya mwaka mzima na sio kutokana michuano ya kombe la bara Afrika pekee'',aliongezea Aubameyang, ambaye anaongoza kwa mabao katika ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani akiwa amefunga magoli 18.

Mchezaji Anayemzidi Lionel Messi Kwa Magoli

ImageGettyImageAritz Aduriz ni wa pili kwa ufungaji mabao Uhispania, akipitiwa tu na Ronaldo

Mashabiki wengi wa kilabu ya Athletic Bilbao wangecheka iwapo ungetaja miaka ya nyuma kwamba Aritz Aduriz angelinganishwa na Lionel Mesii,Cristiano Ronaldo na Luiz Suarez.

Mchezaji huyo anayekaribia miaka 35 ameingia katika kumbukumbu za daftari lenye wachezaji wenye mabao mengi pamoja na Messi,Suarez,Karim Benzema na Neymar msimu huu.

Wale wasiofutilia ligi ya Uhispania huenda wasimtambue Aritz Aduritz ni nani.Aduriz alifunga mabao mawili katika mechi ya ushindi dhidi ya Eibar na kufikisha mabao yake kuwa 25 katika michuano yote msimu huu.

Nyota wa Real Madrid,Ronaldo ni mchezaji pekee anayesakata soka yake nchini Uhispania aliyewahi kufunga mabao zaidi,ijapokuwa Messi,Suarez,Benzema na Neymar wana mabao mengi ukilinganisha na mechi walizocheza dhidi ya Aduriz.

Lakini sio mabao mengi ya Aduriz yaliowavutia wengi,kasi yake ya kuweza kufunga mabao ya 'bicycle kick' dhidi ya Eibar imempa uwezo wa kupigania nafasi ya bao zuri msimu huu na kuweka jina lake katika midomo ya wapenzi wengi wa ligi ya Uhispania.

Ungana na mchezaji wa Atletico Bilbao Aduriz ambaye amefunga mabao mengi zaidi ya Messi.

Aduriz, ambaye atafikisha miaka 35 mnamo tarahe 11 mwezi Februari,amefunga mabao 25 katika michuano yote ya Athletico Bilbao msimu huu.

Mchezaji mwenye mabao mengi nchini Uhispania.Bao katika kila mechi.Cristiano Ronaldo 27 27 1.00Aritz Aduriz 25 34 0.74Luis Suarez 24 28 0.86Karim Benzema 21 20 1.05Neymar 20 24 0.83Lionel Messi 19 23 0.83

Lakini ni vipi Aduriz ameweza kuingia katika orodha ya wafungaji bora katika ligi ya Uhispania?

Kupitia uvumilivu na ubarakala .

Alirudi katika kilabu ya Atletico Bilbao kwa mara ya 3 mwaka 2012,baada ya kufeli kuvutia alipokuwa kijana,ambapo alihudumu misimu miwili na nusu akichezea Burgos na Real Valladolid kabla ya kurudi mwaka 2005 na 2008 ambapo alizuiliwa na uwepo wa Fernando Llorentes.

Athletico ilimchezesha sana Llorentes kuwa mshambuliaji wa pekee hatua iliomaanisha kwamba Aduriz alipatiwa nafasi chache,na baadaye akaelekea Mallorca na Valencia ili kutafuta fursa hiyo.

Lakini mchezaji mwengine maarufu anayeichezea Uhispania, Roberto Soldado alikuwa bora kumshinda na hivyobasi akaamua kurudi Bilbao.

ImageMabao kwa kila mechi

Llorente kwa mara nyengine alijaribu kumzuia Aduriz katika uwanja wa San Mames hatua iliomfungulia mlango katika kilabu ya Juventus.Na mabao 87 ya Aduriz kati ya mechi 161 yameifanya Athletico Bilbao kumsaka mchezaji huyo wa zamani.

Je,anaendeleaje katika Ligi ya Ulaya? Hakuna tatizo.

Aduriz hajakuwa moto wa kuotea mbali kwa mabeki wa Uhispania pekee bali hata katika michuano ya Ulaya.Akifunga mabao sita katika kundi la muondoano la ligi ya Yuropa ,Aduriz anaongoza kwa idadi ya mabao katika kombe hilo la Ulaya.

Rekodi ya Aduriz mwaka 2015-16Mabo aliyofunga katika michuano tofauti.Spanish La Liga 13 20Uefa Europa League 6 8Spanish Supercopa 4 2Spanish Copa Del Rey 2 4Jumla... 25 34ImageAduriz akilinganishwa na washambuliaji wengine wa UhispaniaUchanganuzi wa Mwandishi wa mchezo wa soka nchini Uhispania Andy West

Aritz ni maarufu sana miongoni mwa mashabiki wa kilabu ya Athletico Bilbao,kwa hivyo alikaribishwa vizuri alipojiunga tena na kilabu hiyo kwa mara ya tatu mwaka 2012.

Lakini hata mashabiki wake wakubwa wameshangazwa na uwezo wake wa kufunga mabao katika miaka ya hivi karibuni ambayo yamefuta rekodi yake ya hapo awali.

Amekuwa nembo ya kilabu hiyo akipendwa na kuheshimiwa na wapinzani wake na hivyobasi kuweka kumbukumbu kama mchezaji maarufu wa kilabu hiyo alipofunga mabao matatu pekee au 'hat-trick' katika mechi ya kombe la Super Cup dhidi ya Barcelona na kuipatia kilabu hiyo kombe lao la kwanza tangu mwaka 1984.

Uwezo mkubwa wa Aduriz ni kuruka hewani, ambao umewapa mabeki wengi tatizo kubwa na umemfanya kufunga mabao mazuri ya kichwa.

Kasi ya miguu yake pia imemuwezesha kujitengezea fursa ya kufunga na vilevile ni mchezaji mwenye bidii ambaye anaongoza kwa mfano mwema anapokabiliana na mabeki

Chenge Ndiye Mwenyekiti wa Bunge

Chenge awa mwenyekiti wa Bunge

Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, ambaye aligombea uspika mwaka 2010 akisema anataka

Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge,  akiwaomba wabunge wamchague kuwa mwenyekiti wa Bunge katika kikao cha kwanza cha mkutano wa pili wa Bunge la 11, Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi

Dodoma. Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, ambaye aligombea uspika mwaka 2010 akisema anataka kutibu majeraha yaliyoliumiza Bunge, Taifa na CCM kutokana na kashfa mbalimbali, amechaguliwa kuwa mmoja wa wenyeviti watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Chenge, ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kabla ya kuingia bungeni na kuteuliwa kuwa waziri aliouachia wakati kashfa ya ununuzi wa rada ilipopambamoto, ataongoza Bunge kwa nafasi ya mwenyekiti akiwa na Dk Mary Mwanjelwa na Najma Murtaza, ambao walikuwa wagombea pekee wa nafasi hizo.

Hata hivyo, ilibidi Spika Job Ndugai amuokoe kwa kuzima swali lililohusu kashfa ya uchotwaji wa Sh306 bilioni kutoka akaunti ya Tegeta Escrow lililoulizwa na mbunge kutoka Chadema, Latifa Chande.

Chenge alitajwa kwenye kashfa ya ununuzi wa rada baada ya taasisi ya Uingereza inayoshughulikia makosa makubwa ya jinai, kubaini kuwa alikuwa na dola 1 milioni kwenye akaunti yake iliyokuwa mjini Jersey, fedha zilizohusishwa na ununuzi wa rada hiyo ambayo bei yake ilikuzwa.

Kashfa hiyo ilimfanya Chenge alazimike kujiuzulu nafasi ya Waziri wa Miundombinu mwaka 2008, lakini Novemba, 2010 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ilimsafisha na siku chache baadaye akagombea tena ubunge na kushinda.

Wakati huo aligombea uspika akisema: “Nagombea kiti cha uspika nikiamini kwamba ninao uwezo wa kutibu majeraha makubwa yaliyoumiza Bunge na Taifa, wananchi na chama changu kwa sababu tu ya kuwa kiongozi aliye tayari kujitafutia na kujitwalia umaarufu au ushujaa binafsi kwa njia ya kuwahujumu, kuwaumiza na kuwachafua wengine kwa kutengeneza tuhuma na kashfa za kila namna. Tiba ya uongozi wa aina hii ni kuchagua kiongozi bora wa Bunge.”

Hakueleza kuwa aliyekuwa akimtuhumu ni Samuel Sitta, spika wa Bunge la Tisa ambalo liliboresha kanuni na kuruhusu mijadala moto, hasa ya kashfa dhidi ya viongozi wa Serikali na kusababisha mawaziri kujiuzulu.

Mwaka juzi alijikuta kwenye kashfa ya  Tegeta Escrow baada ya kubainika kuwa aliingiziwa Sh1.6 bilioni na mmoja wa wamiliki wa IPTL na kusababisha apelekwe kwenye Baraza la Maadili la Viongozi wa Umma, ambako alijaribu kulizuia lisimhoji kwa kuomba ufafanuzi Mahakama Kuu, lakini aligonga mwamba na kurejeshwa kuhojiwa.

Kashfa hiyo ilimfanya avuliwe uenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge, lakini alirejea tena bungeni baada ya uchaguzi wa mwaka jana.

Jana, Chenge ambaye aliwahi kujiita “nyoka wa makengeza” wakati wa kashfa ya Escrow, pamoja na wenzake wawili walikuwa wagombea pekee wa nafasi hiyo ya mwenyekiti ambayo hushikwa na watu watatu wanaomsaidia Spika kuendesha chombo hicho cha kutunga sheria.

Mara baada ya Dk Mwanjelwa kumaliza kujieleza mbele ya wabunge na kuulizwa maswali, Chenge alifuatia na alianza kubanwa swali la Mbunge wa Ndanda (Chadema), Cecil Mwambe.

“Katika Bunge lililopita CCM na wabunge walikuwajibisha kwa kashfa ya Escrow na sasa hivi unaomba kuwa mwenyekiti, siku ukiwa unaliongoza Bunge hili na hoja ya hiyo ikarudi bungeni je Utatenda haki katika kulisimamia Bunge? “ alihoji Mwabe.

Huku akicheka, Ndugai alisema hilo siyo swali jambo ambalo liliwafanya wabunge kupinga, huku wengine wakicheka. Hata hivyo alimruhusu Chenge kujibu.

“Bunge linaongozwa na kanuni na pale ambapo inakuja hoja bungeni au katika kamati zetu na inaonekana kuna masilahi fulani au inakuhusu mwenyewe, ni busara tukazingatia kanuni,” alisema Chenge.

“Ni vyema nafasi (ya mwenyekiti) ikashikwa na mwingine ili shughuli za Bunge zisiwe na makandokando yoyote. Ningeweza kusema zaidi ya hapo ila naomba niishie hapo.”

-

Yusuph Manji Amuita Mezani Tajiri Wa Simba

INGAWA uongozi wa Simba umejibu na kufafanua kwa hoja juu ya kupinga uwekezaji wa bilionea,

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji.

ADVERTISEMENT

INGAWA uongozi wa Simba umejibu na kufafanua kwa hoja juu ya kupinga uwekezaji wa bilionea, Mohammed Dewji ‘Mo’, baadhi ya mashabiki wanaonekana kutofurahia hali hiyo huku Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, akiwasihi wakae naye (MO) mezani na kama kuna uwezekano wampe timu akumbane na mziki wake.

Manji anaamini kwamba MO akipewa Simba ushindani utaongezekana na uwekezaji utakuwa mkubwa ingawa atakumbana na changamoto nyingi kuliko anavyodhania ni rahisi akiwa nje ya Simba.

Bosi huyo wa Yanga, ametamka kwamba ujio wa Dewji Simba ungeleta changamoto kubwa ya kimaendeleo kwenye maendeleo ya soka haswa kwa watani wa jadi, lakini hamaanishi kwamba anamhofia.

“Napenda changamoto nimesikia hizo taarifa za ujio wa MO sijajua zimefikia wapi kuna wakati nilisikia ameamua kuachana na huo mpango, mimi namkaribisha wala siwezi kuhofia kwa lolote, napenda changamoto,” alisema Manji ambaye amethibitisha kugombea uenyekiti wa Yanga kwa mara nyingine kwenye uchaguzi ujao.

“Kuna changamoto kubwa katika kufanya mambo ambayo anayataka kwenye Simba, si jambo rahisi lakini naamini hata akipewa Simba bado hawezi kutupa athari zozote sisi kama Yanga,”alisisitiza  Manji na kusema ni jambo zuri kama Simba wakikaa mezani na Dewji na kumpa nafasi akumbane na changamoto za uendeshaji.

AMTAJA HANSPOPE

Manji amedai kushangazwa na hatua ya Simba mpaka sasa kuendelea na Kamati ya Usajili na viongozi wao kuwa na majukumu wakati kazi yao imeshapita. Alisema majukumu ya kamati ya usajili yanafikia tamati ligi inapoanza ambapo kamati hiyo na viongozi wake hawakutakiwa kutumia cheo hicho kwa sasa wakati majukumu yao ya kusajili yalishamalizika.

“Nasikia kuna kamati ya usajili Simba inafanya nini mpaka sasa? Sidhani kama hiyo ni sahihi majukumu yao yalishamalizika. Huoni hapa Yanga mtu anayehusika na usajili anaongea wakati huu,” alisema Manji ambaye maneno yake yameonekana kumlenga Zacharia Hanspope aliye Mwenyekiti wa Kamati ya usajili Simba.